Mauzo na risiti
Rekodi mauzo kwa sekunde. Chagua bidhaa, kiasi, punguzo na njia ya malipo — cash, simu, benki au mkopo. Umekosea? Ghairi mauzo au rekodi bidhaa iliyorudishwa.
Mauzo, stock, matumizi, madeni, wafanyakazi na ripoti — vyote kwenye app moja rahisi. Jua faida yako ya leo, mtaji wako uko wapi, na bidhaa zipi zinakuletea pesa zaidi.
Angalia Mipango na Bei Pakua App kwa Android (APK)Lipa kwa simuData yako mtandaoniInafanya kazi kwenye simu yoyote
Daftari+ inakusanya mauzo, stock, matumizi, madeni na wafanyakazi wako mahali pamoja — ili ujue hali halisi ya biashara yako kila wakati.
Rekodi mauzo kwa sekunde. Chagua bidhaa, kiasi, punguzo na njia ya malipo — cash, simu, benki au mkopo. Umekosea? Ghairi mauzo au rekodi bidhaa iliyorudishwa.
Ona idadi ya kila bidhaa, weka kiwango cha chini, na pata tahadhari bidhaa inapokaribia kuisha. Kila kuongezeka na kupungua kwa stock kunarekodiwa.
Jua mtaji ulio kwenye stock, thamani ya kuuza na faida inayotarajiwa. Pata orodha ya bidhaa zinazouzwa sana, zilizobaki chache, zisizouzwa na zenye faida kubwa.
Ripoti za mauzo, faida na matumizi zinakuonyesha biashara inakwenda wapi — bila kukokotoa kwa mkono au kujaza madaftari.
Andika kila matumizi ya biashara na uone pesa inaenda wapi. Madeni ya wateja yana historia ya malipo — jua nani anadaiwa kiasi gani.
Ongeza wafanyakazi (saler) bila kikomo. Kila saler anaona mauzo yake mwenyewe, na historia ya shughuli inaonyesha nani alifanya nini.
Kila akaunti ina link yake binafsi ya rufaa. Wanaojisajili kupitia link yako wakilipia subscription, wewe unapata kamisheni — hadi ngazi tatu.
Ukishasajili biashara yako Daftari+, unaweza kuomba mkopo wa mtaji moja kwa moja kwenye dashibodi yako. Jaza KYC mara moja, admin akikubali unapokea fedha kwenye simu yako.
Reach ni audience network ya ndani ya DaftariPlus — inayounganisha biashara yako na watumiaji wengine wanaochagua kwa hiari kuiona namba yako na kuipakua wenyewe. Si guarantee ya WhatsApp Status views — ni opted-in contact connections za kweli.
Manunuzi na wasambazaji — gharama za kununua bidhaa zinarekodiwa
Wateja na madeni — historia ya malipo kwa kila deni
Arifa za muhtasari — mauzo na faida kwenye simu yako kila baada ya saa 2
Malipo kwa simu — lipia subscription kupitia PalmPesa
Salama — data ya kila biashara imetengwa na nywila zinalindwa
Historia ya shughuli — ona nani alifanya nini na lini
Hakuna kikomo cha mtaji wala wafanyakazi kwenye mpango wowote. Lipia kwa simu na uanze mara moja.
Bei zinaweza kubadilika. Bei ya sasa inaonekana kabla ya kulipa.
Maoni ya kweli kutoka kwa wafanyabiashara wanaotumia Daftari+ kila siku.
Jisajili kwa email au akaunti ya Google/Apple, weka bidhaa zako, kisha lipia mpango unaokufaa. Malipo yakithibitishwa, subscription yako inawashwa mara moja.
Kupitia PalmPesa. Unaweka namba yako ya simu, unapokea ombi la malipo kwenye simu yako, kisha unathibitisha kwa PIN yako. Ukurasa unaangalia hali ya malipo yenyewe.
Hakuna kikomo. Unaweza kuongeza wafanyakazi (saler) wengi unavyohitaji, na kila saler anaona mauzo yake mwenyewe.
Utaombwa kulipia upya ili kuendelea kutumia Daftari+. Unaweza kulipia moja kwa moja kutoka kwenye ukurasa wa subscription.
Kila akaunti ina link ya rufaa. Mfanyabiashara aliyejisajili kwa link yako akilipia subscription, unapata 5% (ngazi ya kwanza). Wale walioletwa naye wakilipia unapata 3% (ngazi ya pili), na ngazi ya tatu 1%. Unaweza kuomba kutoa mapato kwenye simu yako.
Acha kubahatisha. Rekodi mauzo, fuatilia stock na uone mtaji wako ukikua — kwa simu yako tu.
Kabla hatujaanza, tuambie kidogo kukuhusu: